Mashabiki wa kikosi cha Daring Club Motema Pembe alichowahi kukichezea nahodha wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, wameahidi kuifanyia Simba wema tupu itakapotua Kinshasa nchini DR Congo.
Ahadi ya mashabiki hao inafuatia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Simba itakapoivaa AS Vita wikiendi hii jijini Kinshasa.
AS Vita na DC Motema Pembe ni wapinzani wakubwa. Na mashabiki hao wameahidi kuipokea Simba na kuisaidia kwa kila jambo.
“Waambie Simba waje, tuko tayari na tutafurahi kuwapokea. Tunajua mbinu na mienendo yote ya watu wa Vita,” alisema Allein Mokilin.
Mokilin ameiambia SALEHJEMBE kwamba wao hawafurahishwi na ushindi wa Vita.
“Unajua wao ni wagomvi sisi ni waungwana. Tunajua Simba ni timu kubwa na tutafurahi ikiwafunga hawa watu wagomvi,” alisema.
Katika Kundi D, Simba inaongoza ikifuatiwa na vigogo Al Ahly ya Misri, zote zina pointi tatu na Vita inashika mkia.
Hivyo itakuwa ikipambana kufa au kupona kuhakikisha inapata pointi tatu katika mechi yake ya kwanza ya nyumbani baada ya kupoteza ile ya kwanza ugenini wakilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Ahly.
Badilikeni na aina ya uandishi wenu haujengi fikra za wasomaji zaidi ya kuwapoteza tu na kuonekana hamko professional... Sio lazima muandike habari za kidaku ili mpate readership kubwa. Kule Zambia mlituambi hivi hivi kuwa Simba imepokelewa na timu ya Chama na wamewaahidi kuwapa mbinu ya kuifunga Nkana ugenini matokeo yake Simba wakala kichapo....
ReplyDeleteChange your paradigm please...
Waandishi wetu hawa
ReplyDelete