SALAAM KWA WATANI ZAANZA, ZAHERA AONGEZA MASHINE MBILI TAYARI KUWAUA SIMBA
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameanza kutuma salaam kwa watani zake wa jadi Simba kuelekea mechi ya mzunguko wa pili katika Ligi Kuu Bara.
Zahera amekiri kuwa Simba wapo vizuri lakini hawana sababu ya kuwachukulia poa Yanga ambao wana kikosi cha kawaida.
Kocha huyo kutoka Congo, ametamba kuwa katika kikosi chake atakuwepo mchezaji Mohammed Issa Banka ambaye alifungiwa kutokana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Ujio wa Banka umemfanya Zahera awataje Simba kuwa wajiandae maaana kikosi chake kitakuwa cha moto.
Aidha, Zahera amemtaja mchezaji Gustavo kutoka Yanga B kuwa ni kifaa hatari na anaweza akampa nafasi ya kucheza siku hiyo kwakuwa tayari ameshampandisha kikosi A.
Timu hizo zitaenda kukutana zikiwa na kumbukumbu ya kwenda suluhu ya kutofungana katika mkondo wa kwanza wa ligi.
WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU
ReplyDelete