January 29, 2019


Uwanja wa klabu ya Simba unaojengwa huko Simba umebakisha kidogo kufikia hatua ya kuwekewa nyasi bandia kwa ajili ya timu kuanza mazoezi.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya mafundi katika uwanja huo, Aloyce Joseph, amesema tayari mabomba ya kupitisha maji chini yameshawekwa.

Ameeleza pia, zoezi litakalofuata na kuwekwa kwa nyasi bandia ambazo zitatandazwa chini na baada ya hapo kutawekwa fensi kuzunguka uwanja.

"Mpaka sasa tumeshakamilisha uwekwaji wa mabomba chini na kitakachofuata ni kutandaza nyasi bandia na kisha zoezi la fensi litafuata na timu itakuwa tayari kuanza mazoezi" alisema.

Mpaka sasa Simba imekuwa ikitumia uwanja wa Bocco Veterani kufanyia mazoezi yake katika mechi za ligi na kimataifa kitu ambacho huwafanya watumie gharama kubwa za kulipia.

3 COMMENTS:

  1. Fence muhimu lakini taa zenye viwango bora kwa mzaoezi ya usiku ni kitu cha kuzingatia pia.

    ReplyDelete
  2. WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana aise Mpira ni uwanjani, kwan mlipokuwa vuzuri mlichukua sport pesa? Acha kutapatapa ww.Ujinga wenu yanga ndio unao wamaliza pia ndio unao leta gundu kwenye Mpi
      ra wa tanzania

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic