January 29, 2019


Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima 'Jembe Ulaya, amewatahadharisha Simba kuwa mechi ya watani wa jadi haitabiriki.

Jembe Ulaya amefunguka kutokana na Simba kuichukulia Yanga ya kawaida kwa kipindi hiki huku akiwaonya kuwa wakija na dharau wanaweza kupoteza mchezo huo.

Mchezaji huyo aliyetamba miaka ya nyuma, ameeleza kuwa mechi inayokutanisha Simba na Yanga huwa haitabiriki kirahisi na badala yake yoyote aliyejipanga vema atapata matokeo.

Kuelekea mechi hiyo ya watani wa jadi Malima amesema timu zote mbili zinapaswa kujipanga vema ili kuhakikisha zinacheza kusaka alama tatu.

"Mechi hizi huwa hazina utabiri, unaweza ukaiona Yanga mbovu kwa sasa lakini ikaja ikafanya maajabu zaidi kwa Simba, hivyo timu iliyojipanga vilivyo ndiyo itapata matokeo kwa kutegemeana na namna ambavyo mbinu zitatumika uwanjani" amesema.

2 COMMENTS:

  1. WALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU

    ReplyDelete
  2. Hyu jamaa nae waandishi nao msitupostie vitu vya kifikra kama hv hv huyu Bakali Malima 'Jembe Ulaya' nani kamwambia simba inaidharau yanga nan kasema yanga ni mbovu? Mbovu akaongoza ligi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic