January 13, 2019


Mmoja kati ya viongozi wa benchi la ufundi wa JS Saoura, jana Jumamosi alimvamia mwamuzi Joshua Bondo wakilalamikia bao lililofungwa na mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

Kiongozi huyo akiwa na kipa Khaled Boukacem walimzonga mwamuzi wakilalamikia bao lilofungwa dakika 45 kabla ya mapumziko.

Kwa mujibu wa limewashuhudia kipa na kiongozi huyo wakimzonga mwamuzi mara baada ya filimbi ya mapumziko hali iliyomfanya kocha wa Simba, Patrick Aussems kuingilia kati kabla ya kuja kwa maofisa wa CAF kuwaongezea ulinzi wakati wakitoka nje.

Lakini ulinzi huo haukuweza kusaidia kutokana na kipa huyo kuendelea kulalamika huku wakiwa wanaelekea vyumbani

1 COMMENTS:

  1. TFF ijitathmini namna inavyoendesha soka la Tanzania....kwani kumekuwa na malalamiko ya upendeleo na kuzipangia unafuu ratiba ya mashindano baadhi ya klabu fulani na kuzikandamiza nyingine....sijata timu hizo ila mwenye macho haambiwi tazama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic