ZAHERA ATOA NENO ZITO KWA SIMBA ILI KUEPUKA HAMSA KWA WAARABU
Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Mwinyi Zahera ametoa neno kwa Uongozi wa klabu ya Simba hasa kwa Kocha na benchi la Ufundi kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa barani Africa dhidi ya klabu ya National Alahly ya nchini Egypt. Mechi inayo tarajiwa kupigwa Jumamosi wiki hii.
Akiongea kupitia Azam TV Kocha huyo alisema,"Kocha wa Simba na benchi lake wanapaswa kuwaandaa wachezaji kiakili (mentality) kueleka mchezo huo wa hapo Jumamosi.
"Vinginevyo wachezaji wataingia uwanjani wakiwa na maumivu ya kufungwa kwenye mchezo uliopita ambao walipoteza dhidi ya As Vita ya Congo kwa 5-0. Hivyo suala la kuwatayarisha kiakili ni la muhimu sana vinginevyo wanaweza wakafungwa tena magoli matano tena" amesema.
Simba itakuwa inacheza na Al Ahly Jumamosi ya wiki hii huko Cairo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa na AS Vita kwenye mchezo uliopita.
Kikosi cha Simba kinaondoka leo kuelekea Misri tayari kuzoea mazingira ya huko ili kutohangaika kupata tabu kabla ya mchezo kufika.
Hao simba sasa ni sawa na fikio la kufa huwa halisikii dawa. Simba labda kama watu wanavyosema yakwamba wachezaji wa simba baada ya Manara kusema timu yake inauwezo wa kumfunga yeyote naona kama vile wachezaji wamevimba vichwa nakuanza kulegea mfano wa demu vile nakuanza kuachia badala ya kukaza. Nnaimani kubwa mzungu wa simba kwenye mawazo yake anadhani anadili na maprofeshinali wanaojitambua na hilo ndilo jambo linalomtesa mbeligiji pale simba na atateseka sana. Watanzania sio watu wanaojitambua si kwa wasomi itakuwaje kwa watoto waliokimbia shule na kuangukia kwenye soka? Na ndipo pale simba na uongozi wake unapokosea na kuendelea kukosea kuhusiana na suala la kocha msaidizi. Kwa ulaya sawa muache kocha mkuu atafute msaidizi wake lakini kwa Tanzania hapana uzungu peke yake hauwezi kufanya kazi kwa watumishi wa kitanzania lazima awepo msaidizi mwenye Umagufuli kwenye utendaji wake wa kazi. Watanzania tumelala mno choka mbaya kiakili. Wachezaji wa kigeni wa simba baada ya kuona hakuna hatari yeyote ya ajira zao katika ushindani wa namba kutoka kwa wazawa of course lazima na wao watarelax na kuondosha hali ya kupambana na ndicho kitu kinachoendelea hivi sasa pale simba yuko wapi salamba?. Tunamuona Zahera wa yanga kama muendawazimu katika utendaji wake wa kazi, basi vile alivyo Zahera ni robo tu ya ugumu wa ubora wa kocha anaefaa kufundisha wachezaji wa kitanzania ili wajitambue. Chukulia mfano neema iliyokuwepo azam fc kama ingekuwa timu ya Kenya? Wangekuwepo wapi hivi sasa? Chukulia mfano sapota iliyokuwa nayo timu ya Simba kutoka kwa mashabiki wake na kuwa na bahati hadimu yakuwa na kiongozi muekezaji mwenye mapenzi ya asili na timu yake kama ingekuwa timu ya Kenya au Uganda ingekuwaje? Viongozi wa Simba wanatakiwa wao kumshauri kocha wao kumtafutia kocha wa kiafrica atakaeweza kumsaidia sio tu kufundisha mpira bali pia kudili na tabia za wachezaji wa kiafrica, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zenye wachezaji wa mpira wanaohitaji uangalizi wa karibu karibia muda wote kama vile mtu anaechemsha maziwa. Ningemuomba tu Muheshimiwa raisi Magufuli lile wazo lake la kuunda kikosi kazi cha jeshi cha timu ya mpira chini ya usimamizi wake ni wazo bomba na ndio mpango wa kukata mzizi wa fitina wa kuwapata vijana wa kitanzania wenye ari ya kupambana na kuliondeshea taifa aibu yakuwa taifa la kichwa cha muenda wazimu kwenye medani ya michezo. Wazo lako baba nilitegemea wangetokea wadau wenye fani yao wakalipigia bango lakini kama vile kwenye samaki hakuna wavuvi. Kila la kheri Simba klabu bingwa Africa ila hamuendi kushiriki bali mnaenda kushindana. Makosa mlioanza nayo Congo kwa vita club ya kukubali magoli ya mapema mkirejea kwa Mwarabu basi goli 5 za vita jumlisha nyengine tano 5 hiyo ndio idadi ya magoli ambayo hapana shaka ndio mtakayorudi nayo kutoka Misri.
ReplyDeleteWALE WOTE WANAOIHUJUMU YANGA KUANZIA KWENYE USAJILI KUVURUGA UCHAGUZI WA YANGA KIZUNGUMKUTI, TFF RATIBA KUPANGULIWA KWA KUIUMIZA YANGA, NA HILA ZOTE KWA SUALA LA BENO KAKOLANYA, .......LAANA YAKE NI MPIRA WA TANZANIA KUFA, KUFUNGIWA NA FIFA, SIMBA KUONDOLEWA CAF CL, KUKOSA UDHAMINI WA LIGI, TIMU ZA TANZANIA KUTOLEWA FAINALI ZA SPORTSPESA ...NA MAMBO MENGI KUTOKWENDA VIZURI.....CHANZO NI DHAMBI YA KUIHUJUMU
ReplyDeleteNa wewe wacha kuweweseka misili ya dereva mlevi alienusurika ajali ya gari. Yanga wanaoihujumu ni wanayanga wenyewe bro achana kulishwa fikra pumbavu kuwa kuna watu wa nje ya yanga ndio wanaoihujumu yanga zaidi ni Zambi zake yenyewe yanga wakati wa uongozi wa malinzi chini ya utawala wa Manji jinsi walivyokuwa wakivinyanyasa vilabu vingine kama vile kuwanyan'ganya timu nyengine wachezaji wao kiulahai,kulazimisha ushindi wa mizengwe,kuzishikilia akili za waamuzi kuibeba yanga,kuichakachua ratiba ili kuibeba yanga yaani wakati wa malinzi yanga walitenda zambi nyingi. Kwa hivyo wacha yanga iteseke sasa na bado.
ReplyDelete