AFRICAN LYON WAIRAHISISHIA KAZI SIMBA
Klabu ya African Lyon imeiandikia barua bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) kuomba mchezo wao namba 271 dhidi ya Simba SC uhamishiwe Dar es Salaam.
Lyon wamefikia maamuzi hayo ambapo awali walikuwa wanatumia Uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha kwa mechi za nyumbani.
Mwanzoni Lyon waliandika Barua kuomba mechi zao za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe Sheikh Amri Abeid Arusha na Bodi ya ligi ilibariki maabadiliko hayo.
Taarifa imesema kuwa Lyon inadai mchezo dhidi ya Yanga ambao ulifanyika mkoani Arusha katika dimba la Sheikh Abeid Arusha December 20 na Lyon kufungwa kwa goli moja kwa bila (1-0) walipata hasara kutokana na gharama za kambi.
Ukiachana na kambi, gharama za usafiri na pia makato mbalimbali ilikuwa hasara kwao ndiyo maana wameomba mchezo wao dhidi ya Simba ambao utachezwa February 19 ufanyike katika dimba la Taifa, Dar es Salaam.
Timu za Kiswahili Du shidaa njaaa tupu haya hawayakuayaona?
ReplyDeleteHapo Yanga watasema ilikuwa hujuma kwao!
ReplyDeleteHaya ni madhara ya ukata uliosababishwa na yule Karia kuwa kiongozi wa TFF..
ReplyDeleteHivi wewe kiongozi unaruhusu vipi ligi kuu ya nchi kuanza bila kuwa na udhamini wa maana??
Na kwa uhakika si African Lyon peke yake inayopata taabu.. Msikie kocha wa #Yanga anavyolalamika.. Msikie wa #Lipuli.. Hali siyo nzuri ligi kuu..
Kwa uhakika kati ya mwaka ambao bingwa atapatikana kimagumashi ni mwaka huu!!