February 28, 2019


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na mkurugenzi wa Rockstar, Alikiba amethibitisha kupata mtoto wa kiume baada ya mke wake, Amina kujifungua.

Kupitia ukurasa wa Snapchat msanii huyo amepost picha zikionesha sura na miguu ya mtoto. ikidaiwa mke wake Amina amejifunua jana.

Baada ya muda kidogo msanii huyo ali-post clip fupi ya video ikiwaonyesha watoto wakituma salamu kwa msanii huyo wakimwambi “Hongera kwa kupata mtoto wa kiume na mlinde mtoto kwa ajili yetu.”

Alikiba na mke wake wanasherekea ujio wa mtoto wao huyo ikiwa ni miezi michache tangu kufunga kwa ndoa yao mwaka jana na mke wake amina kutoka nchini kenya.

1 COMMENTS:

  1. Tunakupongeza kwa Mungu kukukirimu mtoto wa kiume. Mongu amjaalie mtoto wa kheri kwa wazee wake, mwenye siha na fahamu nzuri ya hali ya juu na mustakbal wa kila aina ya mafanikio na aliyekamata dini yake. Amin

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic