February 28, 2019



UONGOZI wa Azam FC, unatambua ubora wa kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera na namna anavyoibeba timu yake hali iliyofanya watoe tamko lao namna wanavyopasua kichwa kumpata mbeba mikoba wa Hans Pluijm na Juma Mwambusi pamoja na tetesi za kumpa shavu kocha huyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jafary Maganga amesema mchakato wa kumtafuta kocha unaendelea na katika makocha walioomba ajira kukinoa kikosi hicho hakuna jina la Zahera wa Yanga.

"Wengi wameomba ajira ya kukinoa kikosi cha Azam kwa sasa, ila katika orodha ya majina hayo hakuna jina la kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na presha.

"Tunatambua kazi anayoitenda Zahera ndani ya Yanga, anatimiza majukumu yake kwa kiwango kinachowafanya mashabiki wawe na furaha ila uongozi wa Azam FC haujakaa na kuzungumza naye mpaka sasa, suala la kocha ni gumu linahitaji muda wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa kwa sasa bodi bado inajadili," amesema Maganga.

Matokeo mabovu kwenye ligi yametajwa sababu ya kuwatimua makocha hao kwenye benchi la ufundi ikiwa ni pamoja na kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Simba na kwa sasa ipo chini ya kocha Idd Cheche.

1 COMMENTS:

  1. Akija atatupiwa virago tu Tanzania timu Yanga na Simba tu.Bahati mbaya Azam mnajilinganisha nazo badala ya kujilinganisha na saizi yenu Mtibwa au Kagera Sugar

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic