February 28, 2019



UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa utatumia uwanja wa nyumbani wa CCM Kirumba kuwapeleka darasani wachezaji wa Yanga ili kupata pointi tatu.

Alliance wataikaribisha Yanga ambao ni vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza michezo 25 huku wao wakiwa nafasi ya 7 na wakiwa wamekusanya pointi 36 baada ya kucheza michezo 28.

Kocha mkuu wa Alliance, Malale Hamsini  amesema wanatambua ushindani uliopo na namna kikosi cha Yanga kilivyo bora ila kazi yao ni moja tu kubeba pointi.

"Tayari kwa sasa vijana wameshajibu na mfumo umeanza kueleweka na ndo maana unaona tunapata matokeo chanya, tunaiheshimu Yanga kutokana na uzoefu wao lakini tumejipanga kubeba pointi tatu nyumbani.

"Tutawafundisha namna mpira unavyochezwa uwanjani kwa kuwa hiki ni chuo ambacho kinafundisha mpira, wachezaji wangu wengi bado hawana uzoefu ila wale ambao wapo nao wanaendeleza jahazi kwa kasi," amesema Hamsini. 

5 COMMENTS:

  1. Alliance anashinda game hii tena kwa goli zaidi ya moja.

    ReplyDelete
  2. Alliance anashinda game hii tena kwa goli zaidi ya moja.

    ReplyDelete
  3. Ndo manara alivyokutuma we mkia?

    ReplyDelete
  4. Yanga mnapoteza hii kwa Alliance. Wenzenu Rambaramba wameshafikisha 3 za kupoteza, na hao ndo mnaoshindana nao kupoteza. Hii safari hii ni ya kwenu ya 3.

    ReplyDelete
  5. Nakwambieni nyie yanga kesho lazima mfungwe 2 bila mmesoma kichwa cha habali kinasemaje? Hahahahahahah hatale

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic