Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Mwanza leo tayari kwa kibarua cha mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Alliance FC.
Yanga itacheza na Alliance Machi 2 ambayo itakuwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera amesema ligi ina ushindani na wapo tayari kupambana kwa ajili ya kusaka alama tatu.
Ikumbukwe Yanga ipo kileleni kwa alama 61 nyuma ya Azam iliyo na 50 na Simba ikiwa na 48.
Mechi hiyo inaenda kupigwa huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mechi yake iliyopita dhidi ya Mbao FC
Yanga mnajiamini sana nyie, et tumekuja kuchukua poind 3 mhimu inamaana hawo unacheza nao point 3 hawaztaki au,
ReplyDelete