February 3, 2019


Na George Mganga

Kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Al Ahly usiku wa jana katika Ligi ya Mabingwa Afrika kimezidi kuteka vyombo vya habari mpaka sasa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, leo amefunguka kwa kuwapa pole mashabiki na wanachama wa timu hiyo kufuatia msiba huo mzito.

Manara ameandika katika ukurasa wake wa Instagram akiwapa pole na kuwaahidi mashabiki kuwa hesabu zao zipo katika kupata alama nyumbani katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Msemaji huyo anaamini Simba inaweza ikanyakua alama za Al Ahly na AS Vita pale watakapokuja kucheza Uwanja wa Taifa licha ya kufanya vibaya ugenini.



Wakati huo kikosi cha Simba kinaaanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania tayari kuendelea na ratiba ya Ligi Kuu Bara pamoja na kujipanga na mechi zijazo za CAF ambapo watarudiana na Al Ahly Februari 12 2019.

1 COMMENTS:

  1. Hii kweli inaitwa "Ngoja ngoja ..................". Huku tunazidi kuongeza nafasi ya kupata magonjwa ya Moyo na kuongeza idadi ya wanaokufa kwa presha kutokana na vipigo tunavyovipata Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic