BEKI kiraka wa Simba Erasto Nyoni bado anaendelea kushikilia rekodi yake kuwa mfungaji wa mwisho mchezo wa Simba na Yanga ambapo bao lake alifunga katika msimu wa mwaka 2017/18.
Bao hilo la Nyoni ambalo alifunga kwa kichwa baada ya Shiza Kichuya kupiga faulo dakika ya 36 na kulizamisha moja kwa moja wavuni na kuifanya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 limedumu mpaka leo licha ya timu hizo kukutana kwenye mzunguko wa kwanza.
Simba ilipoikaribisha Yanga Uwanja wa Taifa, kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliopigwa September 30 hakuna timu iliyovunja rekodi ya kichwa cha Nyoni.
Tayari zimepita siku 292 tangu bao hilo lifungwe na leo wanakutana ikiwa ni siku ya 293 huku Nyoni akiwa ameanza mazoezi kutokana na majeruhi hivyo swali la nani atavunja rekodi yake litajibiwa leo Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment