February 21, 2019





Klabu kongwe ya Yanga mambo safi baada ya kufanikiwa kukusanya shilingi Milioni 21.3 kupitia kampeni yao ya kuichangia timu hiyo iliyoanzishwa mwezi huu.

Kama unakumbuka kampeni hiyo ilianzishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongoman, Mwinyi Zahera aliyoianzisha kutokana na mtaji mkubwa wa wanachama waliokuwepo Yanga.

Zahera alianzisha kampeni hiyo baada ya timu hiyo kuyumba kiuchumi tangu aliyekuwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji kutangaza kujiuzuru.

Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa fedha hizo wamezipata kupitia michango wanayoichangia kupitia njia tatu ambazo ni Tigo Pesa, MPesa na bank ya CRDB.

Saleh alisema, kwa kupitia Tigo Pesa wanachama wamechangia Sh mil 5.9, Mpesa Sh mil 6.3 na CRDB Sh mil 9.1 na kufikia Sh mil 21.3.

Licha ya wanachama hao kuchangia, lakini bado hawajafikia malengo yao wanayoyahitaji, hivyo wamewaomba wanachama kuendelea kuichangia timu hiyo ili kufanikisha baadhi ya mahitaji yao.

“Tunawashukuru sana wanachama wa Yanga kwa juhudi zao wanazozifanya katika kufanikisha malengo ya timu yao kwa kuichangia.

“Kwani pamoja na michango hiyo kuipata kwa mwezi huu, lakini bado malengo atujayafikia na badala yake wasichoke waendelee kuichangia timu katika kuiunga kampeni ya kocha wetu Zahera.Hadi sasa, Yanga ndio vinara wa Ligi Kuu Bara wakifuatiwa na Azam FC na Simba.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic