February 21, 2019




Baada ya kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kuvunja mwiko wa kutoifunga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Yanga sasa wameelekeza nguvu katika Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Raha zaidi kwa Yanga, imeongeza nguvu ya wachezaji wawili, Feisal Salim ‘Fei Toto’ na Gadiel Michael waliokuwa wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano walizozipata katika michezo iliyopita ua ligi.

Yanga wanataka kushinda mechi yao dhidi ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Kikosi hicho kimeamua kuondoka na kikosi cha wachezaji 20 na Benchi la Ufundi la timu hiyo likiongozwa na Kocha Mkuu wa Yanga Mkongoman, Mwinyi Zahera kwenda kuimaliza Namungo.

Msafara huo umeondoka leo alfajili umesafiri kuelekea Ruhangwa, Mtwara kwenda kuvaana na Namungo FC.

Keshokutwa Jumapili jioni ndio siku ya kazi na Yanga itakuwa uwanjani dhidi ya Namungo.

Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh amesema kuwa timu yao imerejea jana alfajili ikitokea Mwanza kwa ndege aina ya Air Tanzania kabla ya kesho (leo) alfajili kuanza safari ya kuelekea Ruhangwa kwa ajili ya mchezo huo.

“Maandalizi ya timu yetu yanaendelea vizuri na kikosi kipo fiti kwa ajili ya mchezo wetu huo wa FA, tunafahamu ratiba inatubana, lakini tutajitahidi kuhakikisha tunapata ushindi.

“Timu imerejea leo (jana) asubuhi kutoka Mwanza kwa ndege tukitoka kuvunja mwiko kwa kuifunga Mbao nyumbani, hivyo nguvu na akili zetu tunazielekeza mchezo dhidi ya Namungo.

“Tunatarajia kusafiri kesho (leo) alfajili kwa basi letu tunalolitumia kuelekea huko Ruhangwa tayari kuwakabili wapinzani wetu Namungo, tuna kibarua kigumu katika mchezo huo lakini hatuna hofu tutapata ushindi kutokana na ubora wa timu yetu,”alisema Saleh.

5 COMMENTS:

  1. Safari na basi kwanini sio ndege?

    ReplyDelete
  2. Kwa namungo mbona kipigo kinawahusu watu wa yanga,kikubwa kujiandaa kisaikolojia

    ReplyDelete
  3. Kwa namungo mbona kipigo kinawahusu watu wa yanga,kikubwa kujiandaa kisaikolojia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Mikia FC ninyi mlishatolewa na Mashujaa msubiri mwakani

      Delete
    2. Mnapambana kutafuta nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho; Tunapambana kutafuta nafasi ya kuingia robo fainali ya Kombe la Klabu bingwa Barani Afrika. Hizi ni level mbili tofautiii za timu! Mtaeleza vizuri mkitoka Lindi!.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic