February 18, 2019




BAADA ya kupoteeza pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons Kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam hesabu zao kwa sasa ni mbele ya Coastal Union.

Azam FC wameshindwa kupata pointi tatu kwenye michezo yao mitatu ya hivi karibuni na kuruhusu kupoteza jumla ya pointi saba.

Walianza mbele ya Alliance kwa kuwana pointi moja kisha wakagawana pointi moja na Lipuli kabla ya kuonyeshwa namna ligi ilivyo na Tanzania Prisons ambao walibeba pointi zote tatu.

Mchezo wao dhidi ya Coastal Union utakuwa kesho Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani kutokana na mipango kuwa sawa na tayari  wameanza mazoezi.

Azam FC imecheza michezo 23 wakiwa na pointi 49 huku wababe wakiwa ni Yanga wenye pointi 58.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic