February 18, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa baada ya ushindi mbele ya Yanga mipango yake ni kuona anashinda michezo yake nane ya viporo ili kujiweka katika mazingira mazuri.

Simba wamecheza michezo 16 ambayo ni ya mzunguko wa kwanza huku Yanga wakiwa wamecheza michezo 24 wakiwa tofauti kwa michezo nane na Simba.

Aussems amesema kuwa anajua ushindani uliopo kwenye ligi na namna ambavyo wanabanwa na ratiba ila hesabu zake ni kushinda michezo yake yote.

"Nimewaambia wachezaji wangu, tuna kazi ngumu ya kufanya na tuna michezo nane ambayo ni viporo mikononi ambayo yote ni muhimu kwetu lazima tupambane.

"Kila timu naiheshimu na najua ugumu wa wachezaji wangu ni umaliziaji hilo ni jambo ambalo nitalifanyia kazi na inawezekana kuleta mabadiliko kwenye michezo yangu inayofuata, ninachohitaji ni pointi tu," amesema Aussems.

Simba wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 39 huku wapinzani wa Yanga wakiwa na pointi 58 kesho watamenyana na African Lyon Uwanja wa Amri Abeid Arusha.

1 COMMENTS:

  1. Shauri yao Simba wakileta uzezeta waliouonesha kwenye mechi ya mashujaa wasije wakasema Yanga anazicheza mechi zao. African Lyon yupo kwenye kupigania kutoshuka daraja lazima watakuwa wamejipanga hasa na Simba wakiingia na matokeo yao mfukoni wataadhirika pale shekh Ameri Abeid.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic