February 16, 2019


JOTO la mchezo wa Simba na Yanga limepanda moto ambapo leo itakuwa ni mwisho wa ubishi wa tambo zote za watani wa jadi kwa msimu wa 2017/18.

Hadi kufikia sasa Simba wamecheza michezo 15 ikiwa ni pungufu ya michezo nane kwa Yanga ikiwa imecheza michezo 23.

Katika michezo 15 ya mwanzo kwa Yanga na ile 15 ya Simba msimu huu kuna mengi ambayo yapo nyuma ya watani hao wamefanya kabla ya mchezo wa wa marudio haya hapa:-

Kagere, Makambo wakianza kufunga huchomoki.

Simba wanajivunia Meddie Kagere kwa Simba, alianza kufunga dhidi ya Tanzania Prisons timu ikashinda 1-0. Akafunga tena dhidi ya Mbeya City wakashinda 2-0, JKT Tanzania Simba ilishinda 2-0, Mwadui Simba ilishinda 3-0.

Yanga wanaye Heritier Makambo, alianza mchezo dhidi ya Alliance Yanga ilishinda mabao 3-0, Coastal Union Yanga ilishinda bao 1-0,Lipuli Yanga ilishinda 1-0, JKT Tanzania ikashinda mabao 3-0.

Pia, Amiss Tambwe, kwenye mchezo dhidi ya Singia United Yanga ilishinda mabao 2-0. Tambwe alifunga dakika ya 29 na 45.

Fei Toto mbadili matokeo

Feisal Abdalah 'FeToto' alibadili matokeo katika mchezo wao dhidi ya KMC ambao wengi waliamini utamalizika suluhu, dakika ya 89 walipata faulo ambayo FeiToto alimtungua mlinda mlango mkongwe Juma Kaseja.

Mabao ya Penalti
Mpaka sasa kikosi cha Yanga tayari kimeshinda kwa penalti tatu katika michezo 15 pia wamefungwa bao moja la penalti.

Simba wao wana bao moa la penalti huku nao pia wakifungwa bao moja la penati ambalo lilikua kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC. 

Safu ya ushambuliaji

Simba wao wanamtegemea sana Meddie Kagere kwenye mashambulizi na kuamua matokeo kwani kwenye mechi 15 ana mabao nane kileleni, pia Emmanuel Okwi ana mabao saba hawa ndio ambao ni tegemezi kwa Simba pamoja na Bocco mwenye mabao manne.

Yanga wao tegemeo lao ni Makambo ambaye ana mwendo wa kobe katika ufungaji na katika mechi 15 za mwanzo amefunga mabao nane.

Mkali wa pasi za mwisho

Yanga wao mzee wa miassist, Ibrahim Ajibu ndio baba lao kwenye ligi kwa sasa, kwenye mechi 15 za awali alitoa pasi za mabao 10 na zote akitumia mguu wa kulia.

Simba hapa wanajivunia Clatous Chama ambaye mpaka sasa ametoa pasi nne za mabao katika michezo ambayo wamecheza mpaka sasa.

Uchu wa kufunga

Yanga wakiwa ndani ya uwanja wote wana uchu wa kufunga muda wote kwani wanawatumia mpaka mabeki kupachika nyavu kwa mfano Kelvin Yondani, Abdalah Shaibu hawa ni mabeki lakini wametupia bao moja moja.

Simba wao wana Asante Kwasi ambaye ni beki wa kushoto kutupia, ana mabao mawili mpaka sasa.

Ukiwaacha hawa wanakuliza kwa mabao ya mapema

Mrisho Ngassa wa Yanga anahatari sana kipindi cha kwanza kwani bao lake la kwanza alifunga dakika ya kwanza ilikuwa dhidi ya Stand United Uwanja wa Taifa.

Meddie Kagere wa Simba naye ni hatari kipindi cha kwanza bao lake la kwanza alilifunga kipindi cha kwanza dakika ya pili dhidi ya Prisons.

Wababe wa kupindua meza

Yanga wanashikilia rekodi ya kupindua meza kibabe na kusepa na pointi tatu kwenye michezo ambayo walianza kufungwa, walifanya hivyo mbele ya, Prisons na Biashara United ambazo zilianza kuitungua.Pia walisepa na pointi moja mbele ya Ndanda FC ambao walianza kuwafunga.

Simba bado hawajaweka rekodi hiyo, walifungwa na Mbao dakika ya 26 na Said Khamis kwa penalti hawakuweza kupindua matokeo.

Kadi nyekundu

Wote wameonyeshwa kadi nyekundu ugenini, Yanga mchezaji wao Mrisho Ngassa alionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons mkoani Mbeya
Simba, nahodha John Bocco alionyeshwa kadi nyekundu mkoani Shinyanga walipocheza na Mwadui FC.

Safu imara ya ulinzi

Simba imekuwa makini katika sehemu ya ulinzi kwani katika michezo 15 wameruhusu kufungwa mabao matano pekee huku Yanga wakiruhusu kufungwa mabao tisa katika michezo yao.

Jumla ya mabao ya kufunga

Simba kwenye michezo 15 amejikusanyia mabao 31 ambayo kati ya hayo ni bao moja tu mchezaji wa timu pinzani alijifunga. huku Yanga wakiwa na mabao 29 yote wakiwa wamefunga wao wenyewe.

Nana atamfunga mwenzie

Hapa ni yule atakayetumia makosa ya mpizani wake kwa uhakika ndiye atakayeamua mateko kwani mpaka sasa hakuna wa kumcheka mwenzake kutokana na namna ambavyo matokeo huwa yanakuwa.

Dakika tisini ndiyo zitampata mbabe wa hawa jamaa wa Kariakoo siku ya Februari 16 huku wakiwa na kumbukumbu ya suluhu tasa Uwanja wa Taifa mzunguko wa kwanza.

Kutoka Championi

3 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Umenena Vema Ila Ni Mtazamo WAko Tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio ni mtazamo wake lakini tusubiri mechi pitia blog yangu pia www.chuocharap.blogsport.com

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic