February 7, 2019


KIKOSI cha JKT Queens kimeweka rekodi ya kipekee kwenye Ligi ya wanawake Tanzania, maarufu kama Serengeti Women's Premier League baada ya kucheza michezo 11 ya mzunguko wa kwanza sawa na dakika 990 kwa kufungwa mabao matatu pekee.

JKT Queens ni mabingwa watetezi wamekuwa na safu kali ya ushambuliaji ndani ya ligi ya wanawake, katika michezo 11 wamefunga mabao 72 sawa na wastani wa kushinda mabao zaidi ya matano katika kila mechi.

kocha wa JKT Queens, Ally Ally amesema rekodi hiyo ni ya kipekee anaamini juhudi zaidi inahitajika ili kupata mabao mengi zaidi ya hayo mzunguko wa pili na kufikia lengo la kubeba kombe.

"Ni mabingwa watetezi tuna kazi ya kuendelea kuifanya kwa hali na mali kuona tunafikia lengo la kubaki na kombe letu kama ambavyo tulifanya msimu uliopita," amesema.

Wakati JKT Queens wakiwa ni vinara wa Ligi ya Wanawake baada ya kufikisha pointi 33, Mapinduzi Queens inaburuza mkia ikiwa na pointi mbili baada ya kucheza michezo 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic