MBABE wa washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Emanuel Okwi, Salum Ayee wa Mwadui FC amepania kuweka rekodi mpya leo Uwanja wa Taifa.
Ayee ana mabao nane kwenye Ligi Kuu mpaka sasa akiwaacha Kagere na Okwi wenye mabao 7, amesema wapo tayari kuonyesha maajabu katika mchezo wao wa leo na Simba.
Ayee amesema mafunzo ambayo wameyapata na uzoefu walionao wana uhakika wa kuchukua pointi tatu Uwanja wa Taifa ili kujiweka katika nafasi nzuri.
"Tunaiheshimu Simba na tunajua kwamba wapo vizuri maana tulipokutana nao mzunguko wa kwanza walitufuga mabao 3-1 sasa tumewafuata kulipa kisasi.
"Wachezaji wana morali kubwa ya kupambana na hilo linatufanya tuamini tutafanya makubwa, tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema Ayee.
Mwadui wamecheza michezo 24 wakiwa nafasi ya 16 baada ya kujikusanyia pointi 24 kwenye msimamo wa Ligi kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment