February 8, 2019


KOCHA wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye alishawahi kuinoa Simba, amefunguka kuwa, kikosi hicho kitashinda mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly ya Misri kutokana na mipango inayofanywa na benchi la ufundi la timu hiyo.

Simba walipoteza mchezo wao wa ugenini dhidi ya Al Ahly kwa mabao 5-0, ambapo wanatarajia kurudiana Februari 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kusaka nafasi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Julio alisema uwezo wa kuwafunga Al Ahly ni mkubwa, kutokana na mipango ambayo benchi la ufundi la Simba inaipanga, huku akiweka wazi kuwa mbinu pekee ya kuwaamaliza Waarabu hao ni mipango itakayofanyika nje na ndani ya uwanja.

“Bila mipango wale Waarabu ni ngumu kuwafunga, ila naliamini benchi la Simba lazima litasuka mipango ya ndani na nje ya uwanja ili kuweza kupata pointi mbele ya Waarabu, inawezekana kabisa timu yetu kushinda mchezo huo,” alisema Julio.

2 COMMENTS:

  1. Lakini Mo Dewji na Simba kwa ujumla haya malengo ingawa ni mazuri kuyafikia ni lazima Ligi ya Tanzania ikue na wanaoiendesha waiendeshe kwa weledi mfumo wetu wa ligi, ratiba za mashindano, ubora wa timu za ligi, waamuzi vyote vinachangia....ili Simba ifanikiwe lazima timu za ligi ziwe bora kuipa ushindani....Yanga mbovu mtibwa mbovu ndanda mbovu haitoisaidia Simba katika pale inapopataka

    ReplyDelete
  2. Tumuombe Mungu hakuna linaloshindikana kwa uwezo wake!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic