UONGOZI WA YANGA WAELEZA NAMNA UNAVYOHUJUMIWA NA SIMBA
KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Samweli Lukumay, amefunguka kuwa wapinzani wao wameanza kuwahujumu kwa lengo la kuwavuruga makusudi kutokana na kusambaza maneno yaliokosa ukweli kufuatia matokeo ya sare mfululizo kwenye Ligi Kuu Bara.
Yanga wamekuwa wakihusisha hujuma hizo na mchezo wao wa Februari 16 utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Simba.
Yanga inaongoza ligi kuu ikiwa na pointi 54 ikiwa ikipoteza mchezo mmoja na kutoka sare mbili mfululizo hali iliyosababisha kuwepo kwa taarifa za mgomo baridi wa wachezaji wa timu hiyo uliotokana na viongozi wasiomtaka Mwinyi Zahera kufuatia kuingilia suala la fedha za michango ya timu.
Lukumay alisema mpango huo unafanywa na wapinzani wao wakiwemo Simba kwa lengo la kutaka kuwatoa mchezoni kutokana na kuongoza ligi kwa pointi nyingi.
“Kwanza nikutoe hofu, Yanga hakuna kitu kama hicho na wala wachezaji au viongozi hawawezi kukaa kujenga mipango hiyo michafu, huo ujumbe hata sisi tunauona ukitembea mitandaoni lakini siyo kweli.
“Unajua hapo ni wapinzani wetu ambao wao wanatafuta kila sababu ya kutuondoa kwenye mipango yetu ila kuhusu sare za mikoani uongozi tunaelewa ugumu wa viwanja vya huko na hizo ni hujuma ambazo wamezianzisha,” alisema Lukumay.
Presha imeanza kupanda.Gari la barafu limekutana na jua kali.Visingizio vimeanza.Walipocheza mechi 15 nyumbani hatukusikia kelele za hujuma.Mechi 3 pointi 2 kelele zimeanza.
ReplyDeletePoints 7 zimeyeyuka na jua kali. Kelele nyiiiiingiiiiiiii....... tulijua tu, mlicheka sana kiasi kwamba mkasau kuweka cheko za akiba, sasa mmeishiwa cheko, mmeanza kulia!. Na bado!.
Delete