February 3, 2019


KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameweka wazi kitu kinachomchanganya kwa sasa ni ugumu wa ratiba ya timu yake hasa kwenye ligi kuu ambapo wameachwa nyuma kwa michezo mingi na wapinzani wao.

Simba ambao jana walikuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, wapo nyuma kwa mechi tisa dhidi ya KMC ambao wanashika nafasi ya tatu na mechi sita dhidi ya Yanga ambao ndiyo vinara.

Mbelgiji huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa wanakabiliwa na ratiba ngumu katika ligi kwani wana zaidi ya nusu ya mechi za ligi ambazo wanatakiwa kuzicheza ndani
ya miezi mitatu pekee ambayo imesalia kabla ya ligi kumalizika.

“Tuna ratiba ngumu mno kwa  sasa kwenye ligi kwa sababu ni miezi mitatu tu imebaki kabla ya ligi kumalizika lakini bado tuna zaidi ya mechi nusu za msimu ambazo tunatakiwa kuzicheza.

“Hili ni jambo gumu kwetu na kwa wachezaji kwani nafahamu fika juu ya wachezaji wengi hawawezi hali kama hii, katika ratiba yetu utaona tumepangiwa kucheza kwa tofauti ya siku chache sana hili jambo najua litaathiri kwa namna fulani japo hakuna namna inabidi tupambane vilivyo kuhakikisha tunapata pointi katika mechi zote hizo ambazo zimebaki,” alisema Mbelgiji huyo.

CHANZO: SPOTI XTRA

1 COMMENTS:

  1. Sasa utashangaa Mashabiki Sijui Wanatumia akili Zipi Kufirahia viporo Wakati Kichaga Wao Anaona havifai

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic