February 3, 2019



WACHEZAJI watatu kutoka Tanzania wameiteka Ligi Kuu ya Misri baada ya kupata nafasi kuzitumikia timu hizo na kwa sasa wanafikia idadi ya wachezaji watatu.

Mpaka sasa tayari Tanzania inapeperusha bendera yake kimataifa ikiwa na wachezaji wake watatu ambao ni Himid Mao, Yahya Zayd na Shiza Kichuya.

Himid ambaye ni nahodha msaidizi wa timu ya Taifa alipokuwa bongo alikuwa anacheza Azam FC yeye anakipiga kwenye kikosi cha Petrojet ambacho kwa sasa kimecheza michezo 20 na kinashika nafasi ya 18 kikiwa na pointi 15 baada ya kucheza michezo 20.

Zayd ambaye alipokuwa bongo alikuwa Azam FC yeye yupo na Ismaily huku kikosi chake kikiwa kimecheza michezo 17 nafasi ya 11 pointi 23 na Kichuya ambaye kwa sasa yupo ENPPI kikosi chake kimecheza michezo 20 nafasi ya 14 kikiwa na pointi 21.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic