KAZI IPO, UJUMBE HUU WA MACHUNGU WATUMWA NA MBAO KWENDA YANGA
MBAO FC ya Mwanza, imesema balaa la kufungwa ambalo Yanga imekumbana nalo juzi Jumamosi kutoka kwa Simba, ndilo itakalokutana nalo Jumatano kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Yanga itapambana na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku ikiwa imetoka kuchezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba.
Msemaji wa Mbao FC, Crisant Malinzi, ameliambia Championi Jumatatu kuwa: “Tunaendelea na maandalizi yetu kwa ajili ya mechi hiyo, na lengo letu ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi.
“Kwa hiyo Yanga waje waki jua kabisa kuwa hakuna watakachoambulia katika mechi hii kwani mbinu zao na mipango yao yote kocha wetu, Ally Bushiri anayo na anajua jinsi ya kuwazuia,” alisema Malinzi.
Mbao FC wapo nafasi ya saba wakiwa na pointi 33 wakati Yanga wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 58
0 COMMENTS:
Post a Comment