February 18, 2019


YANGA ni kama imewawekea ubishi watani wao wa jadi, Simba, ni baada ya leo alfajiri kusafiri kwa ndege kwenda kuwafuata wapinzani wao Mbao FC ya mkoani Mwanza.

Hiyo, ikiwa ni siku moja kabla ya Simba jana asubuhi kupanda ndege kuwafuata African Lyon huko Arusha. 

Wakati Simba wakitarajiwa kujitupa uwanjani kesho Jumanne, Yanga wao watavaana na Mbao keshokutwa Jumatano katika michezo ya ligi.

Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, amese wamesafiri kwa Shirika la Ndege la Air Tanzania. Saleh alisema, msafara wa timu hiyo umeenda na wachezaji 20 na viongozi wote wa Benchi la Ufundi la Yanga linaloongozwa na Mkongoman, Mwinyi Zahera.

“Baada ya mchezo wa jana (juzi), wachezaji waliruhusiwa kwenda kusalimia familia zao na leo Jumapili asubuhi timu iliingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Mbao. “Hivyo, timu mesafiri leo Jumatatu alfajiri kwa ndege kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wetu wa ligi na Mbao tutakaoucheza Jumatano hii,” alisema Saleh.

Tayari kikosi cha Yanga kimeshatua salama Mwanza na sasa kinachosubiriwa ni mchezo huo.

2 COMMENTS:

  1. Muwape wachezaji mishahara na posho ili wapate morari ya kucheza , kupanda ndege kutawasaidia nini huku wakicheza na mawazo yakiwa katika familia zao walizoziacha zikihangaika halafu msingizie simba inahujumu mechi zenu . kila mtu acheze mechi zake

    ReplyDelete
  2. TUNATAKA MAELEZO KWANINI MCHEZAJI SIMON GUSTAV HAKUCHEZA NA SIMBA? BAADA YA MECHI NA SINGIDA MCHEZAJI HUYU SIMON GUSTAV HACHEZI TENA KWANINI? MCHEZAJI MZURI KIJANA JUZI ANGEPEWA NFASI. AU UHAMISHO WAKE KWELI HAUJAKAMILIKA? MBONA KACHEZA NA SINGIDA?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic