KOCHA MPYA AZAM NI BALAA KWELIKWELI
WAHENGA waliona mbali sana enzi hizo. Kuna usemi wao wa ‘adui yako muombee njaa’. Yaani unaambiwa Makocha wa Azam wamepigwa chini tu Jumamosi jioni, hata saa haijapita, makocha wameshaanza kutuma maombi.
Sasa nani atakuwa kocha mpya wa Azam? Ndio swali la msingi linalowaumiza vichwa viongozi ingawa wana CV kibao kwenye ‘email’ zao.
Azam FC ilimtimua kocha wake Hans van Pluijm na msaidizi Juma Mwambusi baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba, huku ikiwa haina matokeo ya kuridhisha katika mechi za hivi karibuni.
Meneja wa Azam FC, Phillip Alando alisema, hadi sasa bado uongozi wa timu hiyo haujajua kocha gani umpe nafasi ya kuinoa timu hiyo.
”Bado mchakato wa kupokea CV kutoka kwa makocha mbalimbali unaendelea ambapo hadi jana (juzi) tumepokea CV za makocha 10 na mchakato bado unaendelea, bodi itakaa na kuamua kocha gani apewe nafasi hiyo lakini kwa sasa bado maamuzi hayajafanyika.
“CV hizo zinapitia kwa CEO kisha bodi itakutana kuchagua atakayefaa, lengo ni kuhakikisha anapatikana kocha bora wa kuiongoza Azam FC,” alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar aliyewahi pia kuwa mwalimu wa shule ya msingi.
Tangu Azam FC ipande daraja kucheza Ligi Kuu Bara imefukuza makocha zaidi.
Si iliwahi kudaiwa kuwa Zahera ni miongoni waliotajwa kupendekeza kujiunga au ilikuwa kuipa kijasho kuifundisha yanga au ilikusudiwa kuitoa kijasho
ReplyDelete