KINDOKI AMPASUA KICHWA BEKI TEGEMEO YANGA
BEKI mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kipa wa timu hiyo, Mkongoman, Klausi Kindoki huku akimtaka kutobweteka.
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache tangu kipa huyo aonyeshe kiwango kikubwa cha kuokoa michomo ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Heritier Makambo.
Awali, kipa huyo alikuwa akikaa benchi katika michezo ya ligi na michuano waliyokuwa wanashiriki kutokana na kubezwa kiwango chake lakini juzi alionyesha uwezo wa kushangaza.
Yondani alisema kuwa Kindoki ni kipa mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kudaka, lakini presha ya mashabiki ndiyo imemfanya apoteze hali ya kujiamini akiwa golini.
“Kindoki siyo kipa mbaya ni mzuri na nilianza kumuona tangu alipojiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, kosa kubwa alilolifanya aonekane siyo mzuri ni kupoteza hali ya kujiamini baada ya kufungwa michezo ya mwanzoni, lakini sasa ameshawaonyesha watu kuwa yeye ni hatari sana.
“Anachotakiwa ni kuwajua mashabiki na kuongeza hali ya kujiamini ili akontroo presha kama alivyofanya katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho tulipocheza na Namungo, kikukweli alidaka vizuri,” alisema Yondani.
0 COMMENTS:
Post a Comment