February 9, 2019


Paul Pogba ameifungia timu yake ya Manchester United mabao mawili kuendeleza ubabe wa kucheza bilia kufungwa tangu ilipokuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer katika michezo 11 wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Fulham na kupanda nafasi ya nne.

Pogba alianza kuiongoza Man United dakika ya 14 akimalizia pasi ya Anthony Martial aliyeonyesha ubora wake katika mchezo wa leo, bao lingine lilifungwa na Anthony Martial dakika ya 23.

Jitihada za Fulham kupata mabao kupitia kwa wachezaji wake Luciano Vietto na Andre Schurrle hazikuzaa matunda mbele ya Manchester United baada ya Pogba kufunga bao la tatu kipindi cha pili kwa mkwaju wa penalti.

Inaingia kwenye nne bora tangu kuanza kwa msimu huu wakati Fulham matokeo ya leo yanaiweka nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wakiwa wana pointi kumi na saba wakiwa wamebakiwa na michezo 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic