KIPINDI cha lala salama ni kipindi hatari kuliko vipindi vyote tunavyopitia hasa kwenye ligi zetu ambazo zinasimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na matapeli wengi kujitokeza kuongoza upatikanaji wa matokeo.
Kwa sasa ni muda ambao huamua nani atabeba ubingwa wa ligi kwa upande wa Ligi Kuu Bara na ni nani atakayeshuka daraja baada ya mzunguko wote kukamilika haya mambo kama yakichukuliwa kiwepesi lazima uumie kwani huwa yanaleta usumbufu.
Ipo wazi kwamba hakuna timu ambayo imepanda daraja na ina mpango wa kushuka daraja kwa sasa kila mmoja anapambana ili abaki ligi kuu sasa hapo ndio unaona kasheshe linaanzia hapo.
Kama matokeo ambayo yanapatikana uwanjani yangekuwa hayana ukakasi hapo tungesema tumefika sehemu nzuri ila kiukweli hali ni mbaya mzunguko huu wa lala salama kila mmoja anazungumza vile anavyotaka ama namna ambavyo anaona mwenendo wa ligi unakwenda.
Pia hata kwa wale wa Ligi Daraja la Kwanza nao wamekuwa wakipata shida timu zao kupata matokeo chanya yatakayowasaidia kupanda ligi msimu ujao bado kuna kazi kubwa ambayo inafanyika kupata mshindi.
Sasa ili kupata timu sahihi ni lazima usahihi uanzie uwanjani hali itakayosaidia kupata mshindani wa kweli ambaye kesho akiwa anawakilisha nchi yetu kimataifa kila mmoja aseme anastahili na anapata matokeo chanya kwa sababu alijiandaa kuwa bingwa na amefikia malengo yake anapaswa kupongezwa.
Wakati haya yakiendelea ni wakati wa kuona namna gani pia licha ya TFF kutazama kwa ukaribu muda huu wa lala salama ni wakati muafaka wa kutazama maendelao na maandalizi ya timu yetu ya Vijana chini ya miaka 17 namna watakavyopeperusha bendera kimataifa.
Ambacho kinanifurahisha ni namna ambavyo watanzania wanapenda mpira na kutoa sapoti pale timu zao zinapokuwa zikishiriki kwenye michuano mbalimbali hasa nyumbani sasa tujipange vema kwa ajili ya kuona vijana wetu wakipigana uwanjani kutafuta matokeo na kubeba kombe la Afcon.
Wachezaji watumie vema nafasi ya kuwa mwenyeji kupata matokeo kwani ni fursa adimu ambayo Taifa limepata kwa wakati huu katika mashindano haya ambayo ni mara ya kwanza kufanyika nchini Tanzania.
Hebu fikiria kama kila kitu ni chako kwa nini uache ushindi uwe mikononi mwa wengine, hilo ni jambo baya na tunapaswa tuogope lisitutokee katika muda wa mashindano haya ambayo yanatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Deni la mashabiki ambao watajitokeza kwenye mashindano hayo linapaswa lilipwe na wachezaji wakiwa ndani ya uwanja kwa kupambana na kupata matokeo chanya.
Mashabiki pia ni wakati wenu kuona ni namna gani mtaanza harakati za kuipa sapoti timu yenu ya Taifa hasa inapowakilisha nchi kwenye mashindano ambayo yanafanyika kwenye ardhi ya nyumbani na si ugenini.
Wachezaji kazi yenu ni moja tu uwanjani kutengeneza nafasi na kuzitumia kwa kupata mabao mengi zaidi ambayo yatawanyanyua watanzania kutoka kwenye viti na kusimama kuwashagilia mwanzo mwisho kishujaa.
Kila kitu kwenye mpira kinawezekana iwapo kutakuwa na nia ya kweli kwa wachezaji kutafuta matokeo ndani ya uwanja na kuwafanya wazidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuogopwa na timu pinzani.
Kama timu itaanza kwa kasi kupata matokeo itasaidia kuleta heshima kwa timu pinzani zitakuwa zinatambua zinakwenda kuonana na timu ngumu kiasi gani kuliko kuanza kwa kupokea kichapo hali itakayofanya wapinzani kukuchukulia kawaida.
Kuheshimiwa kuna raha yake, kutafanya timu iingie uwanjani ikiwa na presha ya kufungwa na mwisho wa siku wanafungwa kweli hii itakuwa ni faida kwetu watanzania.
Saikolojia kwenye mpira ina nguvu japo wengi hawatambui kwamba wakati mwingine mwili huchoka kufanya mambo mengine ila kwa kutumia saikolojia utashangaa namna mwili unavyoendelea kupambana.
Ni ile imani ya kujengwa kwamba unaweza kufanya mambo makubwa na kwa kuamini hivyo hicho ndicho ambacho kinakwenda kutokea.
Basi rai yangu kwa wachezaji wa Serengeti kutambua thamani yao kushiriki mashindano haya na thamani ya mashabiki ambao wapo nyuma yao kuwasapoti kwa hali na mali.
Itakuwa rahisi na juhudi kubwa lazima ifanyike kuona namna ambavyo kila mchezaji anacheza na mwenzake wakiwa ni timu na si mtu mmojammoja.
Dunia nzima itafuatilia mashindano haya hivyo ni fursa pia kwa wachezaji kujiweka sokoni na kufanya kazi ambayo itasaida taifa kiujumla.
Wakati tulionao ni sasa na tunaweza kupata matokeo chanya iwapo tutaamua kwa pamoja bila kujali nani tutacheza naye pamoja na uwezo wetu upo vipi kimataifa.
Benchi la ufundi litumie muda wa maandalizi kuandaa kikosi cha ushindani na sio inafika wakati tunaanza kutafuta sababu zakushindwa hilo si sawa.
Kitakachotubeba kwenye mashindano haya ni maandalizi sahihi na wakati sahihi na sio kukurupuka baada ya kushindwa na kuanza kutafuta sababu za kwanini tumeshindwa.
.
ReplyDeleteخدمة السيو والارشفة وتهيئة مدونتك او موقعك لمحركات البحث
اذا كان موقعك بلوجر او ووردبريس خدمة تهيئة المواقع لمحركات البحث لزيادة فرص ظهور موقعك في الصفحات الاولي
تنبيه / فحص موقعك مجانا
تنبيه / المدة و السعر يختلف بناء على احتياج الموقع
ما أقوم بعمله الأتي :
- ضبط الأسم والوصف والكلمات المفتاحية المتعلقة بمدونتك او موقعك داخل الميتا تاج
- عمل باك لينكس - مسك كلمات
- عمل وصف للموقع بالكلمات الافتتاحية المختارة Description Tag
- إعداد خريطة الموقع sitemap وتقديمها لأدوات مشرفي المواقع بشكل سليم
- ارسال روابط مدونتك لجوجل لجعل عناكب محركات البحث بشكل يدوي لتسريع الارشفة
- تحديد وتصنيف واضافة محتوى الكلمات المفتاحية الخاصة بالموقع Meta Keywords
- انشاء ملف ال Robots.TXT الذي يتوافق بشكل كامل مع محركات البحث وال SEO
- اضافة يدوية للموقع فى كل محركات البحث للتأكد تفعيل الارشفة بشكل نهائى
خبير سيو
سيو
seo تعلم
خدمات سيو
تعليم سيو
Dawa Ya Moto Ni Moto Ngoja Sisi Tukujibu Kwa Lugha Yako خبف
Deleteدسبجدب جبستج دسبجفب دسبج دستج ش جح فبجفف دسجبف دسبجفب د ب ب ب شب دبج دش سبس سبفن سفسب ذس دجب دبسف دبج بج دبجسبفجفبس ذجبف دجبدسب
Siku Nyingine Kama Huwezi Kiswahili Utoe Maoni Kwa Kiingereza