February 28, 2019

BAADA ya kocha aliyeachiwa mikoba na Hans Pluijm pamoja na Juma Mwambusi, Idd Cheche wa Azam FC kutinga hatua ya nane bora ya kombe la Shirikisho mtihani wake wa kwanza Ligi Kuu Bara ni kesho.

Azam itakaribishwa na African Lyon kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza jahazi bila uwepo wa Pluij  kwenye benchi.

Cheche amesema kuwa anawatambua vizuri wachezaji wake na anajua namna ya kuwatumia hivyo hana mashaka katika kazi yake.

"Nawatambua wachezaji wangu kutokana na uzoefu nilionao hapa kwenye kikosi sina mashaka naamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema Cheche.

Kwa mujibu wa mratibu wa Azam FC, Philip Alando kuhusu mchakato wa makocha amesema zaidi ya maocha 10 wameomba kazi kwa kutuma CV zao kwenye email hivyo watazipitia ili kujua nani atabeba mikoba ya Pluijm.

1 COMMENTS:

  1. Wakale wamesema samaki akioza usimtupe, umfanyie viungo umkaushe, atakuja kumuokota mwenzio ulie uje ujute

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic