February 28, 2019


KOCHA Msaidizi wa Singida United, Fred Minziro, jana kwenye Uwanja wa Sokoine ameanza kukaa benchi kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mbeya City kwa kufungwa bao 1-0.

Miziro ameongezwa kwenye benchi la ufundi baada ya kocha  mkuu, Dragan Popadic kusimamishwa kuongoza timu kwa michezo mitatu kwa kosa la kumzonga mwamuzi kwenye mchezo wao dhidi ya Ndanda.

Minziro aliipandisha Singida United Ligi Kuu kabla ya kupigwa chini amerejeshwa na uongozi ili kuendeleza gurudumu la kuinoa timu hiyo.

Nahodha wa Singida United, Nizar Khalfan amesema hawezi kutoa maoni kwa mwalimu wao mpya kwa kuwa bado hajakaa na timu muda mrefu.

"Tumejituma kutafuta matoko ila tumekwama, uwepo wa mwalimu wetu bado siwezi kuzungumzia kwani hatujakaa naye muda mrefu.

"Mtindo uliopo kwa sasa ni kubebana nyumbani, nadhani kuna kampeni ya kila timu ishinde nyumbani, hicho ndiyo kilituponza ila tutaendelea kupambana," amesema Khalfan.


1 COMMENTS:

  1. Hata Yanga ilikataliwa goli halali la Matheo Anthony pale Singida

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic