February 28, 2019




BAADA ya Mtibwa wa Sugar kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union, uongozi wa Mtibwa Sugar umesema wamezinduka upya mwaka huu.

Mtibwa haikuwa na matokeo chanya katika michezo yake ya mwanzo, ilianza mwaka kwa kupoteza mbele ya Prisons (1-0), Mbeya City (1-0), Lipuli (1-0) ikalazimisha suluhu na JKT (0-0) Ndanda (0-0) ikalazimisha sare na African lyon  (1-1) kabla ya kupoteza kwa  Biashara United (2-1) Mwadui (1-0) na  KMC (1-0).

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobas Kifaru amesema mfululizo wa matokeo mabaya ulikuwa unawapasua kichwa hali iliyowafanya wakae na wachezaji, hivyo kwa sasa wanaona mwanga.

"Hatukuwa na matokeo chanya kwenye michezo yetu iliyopita hivyo wa sasa naona kuna kitu kipya kinakuja kizuri kwa ajili ya mashabiki wetu na wadau wa soka.

"Upinzani ni mkubwa nasi tunajitahidi kuongeza juhudi, lengo letu kubwa kwa sasa ni kuona tunarejea kwenye nafasi za juu huo ndio mpango wetu mkubwa," amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar inashika nafasi 12 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza michezo 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic