MTAMBO WA MABAO SIMBA WAMWAGA NOTI HIZI IRINGA
Unaweza kusema mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere kawatajirisha wauzaji wa jezi mkoani hapa kufuatia jezi yake kuuzwa kwa wingi.
Licha ya uwepo wa jezi nyingi za Simba na Lipuli, lakini mashabiki wengi walikuwa wakiinunua jezi ya Kagere jambo ambalo wauzaji walilifurahia sana.
Hali hiyo ilitokea muda mchache kabla ya jana Simba haijacheza na Lipuli kwenye Uwanja wa Samora uliopo hapa Iringa ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Championi ambalo lilipiga kambi katika eneo ambalo jezi hizo zinauzwa nje ya Uwanja wa Samora, lilishuhudia mwanzo mwisho uuzaji wa jezi hizo ukienda kwa kasi.
Mmoja wa wauzaji wa jezi hizo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alisema: “Jezi hapa zinauzwa kwa bei tofauti, hizi za Simba Sh 25,000 na za Lipuli Sh 15,000. Lakini huwezi amini jezi ya Kagere ndiyo inanunuliwa sana. Hapa kila mmoja ameuza si chini ya jezi 20 za Kagere.”
0 COMMENTS:
Post a Comment