MWANACHAMA YANGA: KOCHA SIMBA ALIPASWA KUFUKUZWA KAZI
Na George Mganga
Mwanachama na shabiki lialia wa Yanga, Edgar Chibula amesema kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems alipaswa kufukuzwa kazi kuifundisha timu hiyo.
Chibula ameeleza kuwa ushindi dhidi ya Al Ahly umemuepusha kuondoshwa akiamini mabosi wake walikuwa wanampigia TIMING tu na angepoteza ingekuwa ndiyo safari yake.
Kwa mujibu wa Radio One, Chibula amefunguka kuwa licha ya kupata matokeo, Aussems angepoteza kibarua chake endapo angetoa sare na kisha kupoteza mchezo ujao wa ligi dhidi ya Yanga.
Mwanachama huyo ameweka jeuri mbele kwa kuamini Yanga itaweza kufanya maajabu kwenye mechi hiyo Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
"Unajua Kocha wa Simba ana bahati sana, ilikuwa ndiyo safari yake endapo angefungwa na Al Ahly Ligi ya Mabingwa Afrika, na kama angebaki, basi Yanga tungemfungashia mizigo yake kwa maana Jumamosi lazima tuchukue pointi 3" alisema.
WEWEEEE SUBIRI BASI JUMAMOSI IFIKE
ReplyDelete