February 14, 2019


REKODI zinaonyesha kwamba beki ya Yanga iliyo chini ya Kelvin Yondani kwenye Ligi Kuu Bara imekuwa uchochoro. 

Kwenye michezo 15 ya mwanzo wa ligi ambayo Yanga walicheza sawa na michezo ya Simba waliyonayo kwa sasa tayari walikuwa wameruhusu kufungwa mabao 10.

Licha ya kushinda michezo yao yote kwa wakati huo kutokana na safu makini ya ushambuliaji bado wamepotezwa na Simba kwa upande wa mabeki. 

Beki ya Simba ambayo ipo chini ya Muivory Coast, Pascal Wawa, kwenye michezo 15 waliyocheza wameruhusu mabao matano pekee.

Hivyo Februari 16 kutakuwa na vita mpya ya kulinda rekodi ama kutibua rekodi kutokana na mazingira ya mchezo ambavyo yatakuwa.

5 COMMENTS:

  1. beki ya simba imeruhusu magoli kumi katika michezo miwili iliyofuatana na hapo unaweza kusema ndiyo uchochoro

    ReplyDelete
  2. Amezungumzia kwenye ligi ya ndani
    . Sijajua Yanga ipo kwenye kundi gani kwenye ligi ya mabingwa ya Afrika?

    ReplyDelete
  3. unataka kujua yanga ipo kwenye ligi gani angalia miaka minne ya nyuma mlikua ligi gani ya kimataifa kama sio matopeni na hao Ahli walishafungwa na Yanga Dar kisha Yanga wakafungwa kwa tabu Misri 2-1 mshindi akapatikana kwa matuta

    ReplyDelete
  4. Miaka 4 ya nyuma mkafika wapi?
    Kufungwa na Zanaco nä Township Rollers ndio historia unayotaka kukumbuka?Kufungwa nyumbani na Gor Mahia tena 3 ndio unachokumbusha?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic