ZAHERA ATEMA CHECHE TENA TFF, ATAKA MAAGIZO HAYA YAFANYIKE
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuongeza umakini katika usimamizi wa ligi ili apatikane bingwa halali.
Zahera alisema ligi ya Tanzania ni bora lakini imepoteza ushindani kutokana na mambo ya ovyo yanayoendelea kufanyika ndani ya ligi na kupelekea kupunguza ushindani.
“Hiyo haina ubishi kama ligi itachezwa kwa haki na usawa basi timu yoyote itakayokuwa bingwa basi itafanya vizuri ndani na nje ya nchi lakini kwa mfumo wa sasa wa ligi ni ngumu kupatikana mwakilishi mzuri “ alisema Zahera.
Mkongomani huyo alisema utakuta waamuzi wanachezesha huku wakilazimisha timu A ifunge timu B wakati hawana uwezo.
“Kuna nchi ambazo zinawashiriki zaidi ya watatu katika mashindano ya Kimataifa kama DRC Congo, Misri, Zambia pamoja na Morocco ambapo mbili zinacheza ligi ya mabingwa Afrika na moja au mbili zinacheza Kombe la Shirikisho hayo ndiyo maendeleo ya soka,”alisema Zahera.
Alisema inatakiwa kufika kipindi Biashara United kuifunga Yanga SC au Simba SC isiwe stori lichukuliwe kama tukio la kawaida kwenye soka
Zahera Fanya Kazi Yako Mambo Mengine Haya Kuhusu Mbona Goal La Emanuel Okwi Lilikataliwa Katika Mechi Ya Simba Na Yanga Na Nakumbuka Osman Kazi Ktk Kipindi Cha Kipyenga Cha Mwisho Cha Azamtv Alisema Lilikuwa Goal Halali Na Bado Mech Ya Simba Na Lipuli Lilifungwa Likiwa Halali Lakin Lilikataliwa Na Mwamuzi Lakini Kocha Wa Simba Sijasikia Lalamiko Lolote Wala Uongozi Haukusema Lolote Acheni Majungu Pigeni Kazi Kawape tena Wachezaji Wako Mbinu Ya Kulinda Wakati Beno Hayupo Uone Kitakacho Kupata
ReplyDeletehuyu sasa ni mwimba ngonjera na si kocha maana kama, kocha kama wa azam katoa sare nyingi lakin ukimsikiliza yeye anasema ndo ligi lakin yeye hataki kutoa hata sare sasa amekuwa ni kutoa vitisho tuuuu da sasa nan wa kumuogopa, kwani mbona simba inanyanyaswa weee magoli kama bocco yako ndani lakin refaree anakataa sasa huyu yeye ni nan haswa subiri bado hujaenda Mara, hujaenda mwanza utakoma kama ulujua unakuja ukijua ni yanga tu ndo inacheza umechemka kwakweli maana hata haoni watu wamenyamazia tu da hadi kero zahera zahera zahera da
ReplyDeleteKukataliwa magoli sio kwamba mwamuzi anataka timu fulani ifungwe lahasha; wewe unapata nafasi ya kulirudia goli kwenye replay za tv wakati mwamuzi anacheki move moja tu, ndiyo maana wenzetu ulaya wameamua kuingiza mfumo wa VAR.
ReplyDeleteSuala la nchi kuwa na wawakilishi wengi inategemea tunaishia hatua gani. Mfano: simba mwaka huu wakifanikiwa kuingia robo fainali mwakani tutaingiza timu tatu CAF, 2 clab bingwa, moja shirikisho.
HUYU KOCHA ANAONGEA MNO KILA SIKU YEYE TUUU
DeleteTATIZO VIONGOZI YANGA WANAMUOGOPA YEYE KWA SASA NDIO KILA KITU WAKIMSEMA KUMPA MUONGOZO ANATISHIA KUWAACHIA TIMU ANASUSA HILO NDIO TATIZO KWA SASA KOCHA HUYU HAKUNA WA KUMWELEKEZA ANAFANYA ATAKALO NDANI YA YANGA
DeleteWachangiaji mnachangia kishabiki sana.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteTFF Tunapofikia hatua ya kucheza Simba na Yanga ingieni gharama leteni waamuzi wote 3 kutoka nje ya nchi. Siku zote nani hajui Kwambaa YANGA ndio wanabebwa na marefa wa TZ, leo huyu Kocha analaumu tuu kila kukicha wakati timu yake ndio huwa inabebwa na waamuzi. Nani hajui?? Sasa TFF leteni Waamuzi kutoka nie ya nchi Msumbiji, Malawi, Zambia, Misri, Sudan, Namibia, wala isiwe Afrika Mashariki. Kocha lazima aelewe unawakatisha tamaa marefarii ni binadamu kama wewe, mbona wewe unayo mapungufu yako? Kindoki umemsajili lakini hakustahili, Kakolanya umemuadhibu maisha lakini ndiye golikipa nambari wani n.k
ReplyDeleteReplyDelete
Ninahisi Zahera ana wasiwasi na kuna mnongono kuwa wamechafuwana na Yondani na ijapokuwa wanakanusha, lakini inaaminika hasa toka aliponynganywa ukepteni Yondani inaonesha hana furaha na huku ndio wanamhitajiab
ReplyDeleteLeo wameshikana mashati na Zahera amekaririwa akisema hawezi kubabaishwa nä mtu mdogo. Timu imebidi irudi Dar leo badala ya kesho.
ReplyDeleteHuyu jamaa anaimba sana, huko ndiko kuomba "POO".
ReplyDelete