February 15, 2019


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mchezaji na beki wake, Abdallah Shaibu 'Ninja' atahusika katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Yanga itakuwa mwenyeji Februari 16 Jumamosi ya wiki hii katika dimba la Taifa ambapo itakuwa inawaalika watani zao wa jadi Simba kusaka alama tatu muhimu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga kupitia Radio Magic FM, Dismas Ten, amesema Ninja atacheza kama endapo Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera atampendekeza na akikanusha kupewa adhabu yoyote na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Awali kulizuka taarifa kuwa TFF kupitia Bodi ya Ligi wamemfungia Ninja michezo mitatu kwa kitendo cha kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Coastal Union katika mechi ambayo ilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya mabao 1-1 huko Mkwakwani, Tanga.

Ten ameeleza kuwa hawana barua rasmi juu ya kifunga hicho na wanachotambua ni kuwa ni mmoja wa wanaopaswa kucheza dhidi ya Simba Jumamosi.

"Hakuna barua rasmi inayoeleza kuwa Ninja amepewa adhabu ya kifungo cha mechi 3, hivyo Ninja mpaka sasa atahusika katika mechi ijayo dhidi ya Simba endapo Mwalimu ataamua atumike" alisema.

2 COMMENTS:

  1. acheze mpira sio kuumiza bila mpira

    ReplyDelete
  2. ACHEZE TU ISIPOKUWA AUCHEZE MPIRA SIO KUWATIA VILEMA WACHEZAJI WA TIMU PINZANI CHEZA MPIRA SIO KUWAUMIZA WENZAKO

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic