MWINYI Zahera kocha mkuu wa Yanga atakutana na Simba, Februari 16 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa marudiano, mzunguko wa kwanza walitoka suluhu ya bila kufungana mwenyeji alikuwa ni Simba.
Katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara Zahera aliamua kuwaanzisha benchi mastaa wake wengi kwa lengo la kuwapumzisha na kuwalinda na majeruhi ikiwa ni maalumu kwa ajili ya mchezo wa Simba.
Mchezo wake dhidi ya Coastal Union aliwaweka benchi Papy Tshishimbi, Haruna Moshi, Deus Kaseke, Haji Mwinyi, Klaus Kindoki na Juma Abdul.
Pia mchezo wake dhidi ya Singida United aliwaweka benchi wachezaji wake kama Ibrahim Ajibu, Pius Buswita, Said Juma, na Andrew Vincent na katika mchezo huo alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Kelvin Yondani na Ibrahim Ajibu.
Pia kwenye mchezo wake dhidi ya JKT Tanzania Zahera aliwaanzisha benchi wachezaji wake nyota kama Kelvin Yondani, Matheo Anthony, Deus Kaseke, Mohamed Issa 'Banka' Haruna Moshi 'Boban' , Juma Abdul na Klaus Kindoki.
Zahera amesema kuwa anawaanzisha benchi wachezaji wake wengi muhimu ili awaweke fiti kwa ajili ya michezo yao inayofuata ambapo ni pamoja na ule wa Simba.
"Tunacheza michezo mingi mkoani na tuna mechi nyingi ngumu hivyo nachofanya nawapumzisha wachezaji wangu ili wapate kuwa fiti muda wote kutafuta pointi tatu," amesema.
Ahsante kwa hill msemaji was yanga,maana sasa huyu so kocha Bali msemaji na mfadhili,atamkumbuka kakolanya,na ndiyo mwisho was ubabaishaji wake,yanga ikishinda safi,ikifungwa mar
ReplyDeleteZahera siyo mbambaishaji kama unavyofikiria anafuata weledi.
ReplyDeleteTatizo huelewi nn anafanya pale Yanga ukitaka kujua hilo aondoke then timu aichukue kocha mwingine uone kitakachotokea pale.
Inawezekana una mahaba na Kakolanya or vinginevyo lkn Zahera yupo sahihi kwa swala la Kakolanya na hata sasa hivi akifungwa na Simba hakuna kitakachotokea kama unavyofikiria.
Beno alikuwa anatimiza majukumu yake kama mchezaji siyo kama alilipwa zaidi eti ndiyo ajitume.
Fikiria kwa kutumia kichwa na siyo kiungo kingine cha mwili.
Na hiyo kesho wapumzishe pia kwasababu huko mbeke kuna timu ngumu zinakungojeeni
ReplyDeleteNa vipi ilikuwa Manji arejee yanga mwezi uliopita, vipi keshatuwa?
ReplyDelete