February 15, 2019


SIMBA ikipata pointi nne tu kwenye mechi zake mbili zilizosalia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa na uhakika wa Sh.Bilioni 1.5. 

Mpaka sasa Simba ina uhakika wa Sh.Bilioni 1.3 kwa kufuzu makundi hayo ya Afrika lakini kila inavyozidi kusogea juu inazidi kuongeza furushi.

Lakini mbali na Sh.Bilioni 1.5, Simba watakuwa wamejihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika. 

Simba chini ya muwekezaji Mohammed Dewji ‘Mo’, inacheza na JS Saoura ugenini Machi 9 na kumalizia shughuli nyumbani dhidi ya As Vita ambayo mpaka sasa haijaambulia walau sare ugenini.

Kwa hesabu za kundi hilo zilivyo, Simba inahitaji japo sare ugenini na kushinda mechi yake ya mwisho nyumbani ili kutimiza pointi nne ambazo zitatosha kuivusha. 

“Kundi liko wazi baada ya sisi kufi kisha pointi sita, na nadhani Ahly walitudharau baada ya kutupiga zile bao tano kwao.

"Sasa sisi tulichofanya ni kuwaonyesha kwamba hii siyo timu ya kijijini ni timu inayoheshimu mpira. 

“Tutazicheza kwa akili sana hizi mechi mbili zilizobaki, nina imani sana kwamba sasa wachezaji wameshakaa sawa na njia ya kwenda robo fainali inaonekana kabisa,”alisisitiza Patrick Aussems ambaye ni Kocha wa Simba.

Ahly anayeongoza kundi kwa pointi saba anahitaji ushindi mmoja tu kufi kisha pointi 10 ambazo zitampeleka robo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic