February 21, 2019


TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 inaendelea na kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Afrika kwa Vijana U 17.

Tanzania ni mwenyeji wa AFCON mwaka huu ambazo zinatarajiwa kuanza mwezi April mwaka huu, Serengeti inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Aghakhan, jijini Arusha.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dr Harrisson Mwakyembe alizindua nembo maalumu itakayotumika kwenye fainali hizo Februari 14 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi.

Serengeti ipo kundi A ikiwa ni pamoja na Nigeria, Angola na Uganda huku lile B likiwa na Guinea, Cameroon, Morroco na Senegal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic