February 6, 2019


KOCHA mpya wa Singida United, Mserbia Dragan Popadic na Dusan Momcilovic ambaye ni Kocha Msaidizi waliwahi kuifundisha Simba, leo watakuwa na vita kali na Yanga ya kutafuta rekodi kwenye michezo yao ya Ligi Kuu Bara kulipa kisasi cha mabao 2-0 waliyofungwa Taifa.

Mchezo wa leo utakuwa ni wa tatu kwa Popadic kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kuongoza michezo miwili baada ya kupokea mikoba ya Hemed Morroco.

Katika michezo hiyo miwili alifungwa mchezo wake mbele ya Mbao bao 1-0 uwanja wa CCM Kirumba na mchezo wake wa pili alishinda mbele ya African Lyon mchezo uliochezwa Namfua.

Yanga ya Mwinyi Zahera wanaingia kazini leo wakiwa wanakumbukumbu ya sare dhidi ya Coasta Union huku Singida United wanakumbukumbu ya shindi.

1 COMMENTS:

  1. Hakuna vita hapo nani asiejua kuwa hao ni wateja wa yanga. Yanga hapo anakwenda kujichukulia point tatu zake na kuondoka. Singida walianza vizuri kama timu hapo awali lakini kitendo cha kujifanya tawai la Yanga ndio chanzo cha kufulia kwa singida na wasipobadilika wataishia kama Toto Africa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic