NAHODHA wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu ambaye aliteuliwa na kocha mkuu, Mwinyi Zahera akipokea mikoba ya Kelvin Yondani mpaka sasa tayari ameonja chungu na tamu ya unahodha wake.
Ajibu ameongoza michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara, alianza kazi Uwanja wa Taifa dhidi ya Mwadui FC timu yake ilishinda kwa mabao 3-1.
Mchezo wake wa pili ilikuwa dhidi ya Stand United timu yake ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza ichezo 19 bila kufungwa ilifungwa bao 1-0.
Katika mchezo wa tatu Ajibu aliongoza dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Tanga timu yake ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Kwa matokeo hayo nahodha Ajibu ameweza kuonja chungu na tamu ya unahodha kwa kupata matokeo yote matatu ya kufunga, kufungwa na kutoa droo na mchezo wake wa nne itakuwa leo dhidi ya Singida United.
0 COMMENTS:
Post a Comment