KOCHA wa Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa kikosi cha Simba kinahitaji maboresho makubwa ili kifanye vema kwenye michezo yao ya kimataifa hasa katika safu ya ulinzi ambayo inaonekana kushindwa kufanya kazi yake kwa umakini.
Simba inawakilisha Taifa kwenye michuano ya kimataifa na imecheza michezo mitatu ya hatua ya Makundi ikishinda mabao matatu na kufungwa jumla ya mabao 10 katika michezo miwili.
"Wachezaji wanapaswa watambue wanaiwakilisha nchi kimataifa nao wana nafasi ya kujituma kwani kufanya kwao vizuri ni kwa manufaa ya taifa wakivurunda wanaleta hasara pia kwa taifa.
"Benchi la ufundi linapaswa liangalie kwa ukaribu sehemu ya ulinzi namna ya kufanya maboresho ili wasiruhusu mabao mengi kwani kufungwa sana kunamanisha kuna njia ya kupita hasa kwa upande wa mabeki, nafasi ya kufanya vizuri ipo kwani kundi lao bado lipo wazi," amesema Matola.
Simba wanatarajiwa kucheza na Al Ahly ya Misri ikiwa ni mchezo wa marudio utakaochezwa Februari 12 Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment