February 21, 2019


USHINDANI kwenye ligi unazidi kushika kasi ambapo jana michezo minne ilichezwa na timu nne ziliibuka na ushindi huku nne zikipoteza na kufanya baadhi ya timu kushuka kwenye nafasi zao kama hivi:-

Mbeya City ilifungwa na Tanzania Prison bao 1-0, kabla ya mchezo ilikuwa nafasi ya 11 kwenye msimamo na baada ya mchezo inashuka mpaka nafasi ya 15 ikiwa na jumla ya pointi 30 imecheza michezo 25.

Mtibwa Sugar ya Morogoro baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya KMC, kabla ya mchezo ilikuwa nafasi ya 14 baada ya mchezo inashuka mpaka nafasi ya 17 ikiwa na pointi 29 imecheza michezo 24.

Lipuli ya Matola kabla ya kufungwa mabao 3-2 na Stand United ilikuwa nafasi ya nne kwenye msimamo na baada ya kichapo hicho inashuka mpaka nafasi ya tano ikiwa na pointi 38 imecheza michezo 27.

Mbao FC kabla ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Yanga ilikuwa nafasi ya sita  licha ya kipigo hicho bado imekomaa nafasi ya sita ikiwa na pointi 36.

Singida United kabla ya mchezo wa jana ilikuwa nafasi ya 15 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Ndanda FC inashuka mpaka nafasi ya 18 ikiwa na pointi 29 imecheza michezo 29.

Kwa timu zote zilizocheza jana Singida United inashuka kwa kasi pamoja na Mtibwa Sugar ambayo mzunguko wa pili haijawa na matokeo chanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic