TSHISHIMBI AONGEZEWA THAMANI YANGA
KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongoman, Mwinyi Zahera ametamka kuwa huyu wa sasa ndiye kiungo wake halisi, Pappy Tshishimbi anayemjua na si yule aliemkuta klabuni hapo.
Kiungo huyo hivi karibuni amerejea kikosini akitokea kwenye majeraha ya goti ambapo awali alikosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na kutoridhishwa na kiwango chake.
Tshishimbi alianza kurejesha kiwango chake na kupata nafasi ya kucheza kwenye mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania kabla ya baadaye kudhihirisha ubora wake dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kumdhibiti kiungo Mzambia, Claytous Chama.
Zahera alisema hakuwahi kuwa na ugomvi na Tshishimbi huku akitaja kushuka kwa kiwango chake ndiyo kulisababisha apoteze nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza.
“Tshishimbi niliwahi kumsema mbele ya waandishi ya habari kuwa anacheza bila kufuata maelekezo yangu kutokana na nafasi yake anayoicheza namba sita, hatakiwi kupiga chenga na kukaa na mpira muda mrefu.
“Lakini yeye alikuwa akipiga chenga kitu ambacho nilikuwa sikitaki, yeye kazi yake ni kunyang’anya mipira na kupiga pasi kwa washambuliaji pekee ndani ya wakati ili kuhakikisha timu inapata ushindi.
“Kama unamfuatilia vizuri Kante (N’golo) yule kiungo wa Chelsea anavyocheza utakuwa umenielewa ni mchezaji ambaye haumuoni akikaa na mpira kabisa, kwenye michezo ya hivi karibuni nimeona ubora wa Tshishimbi anaweza kuisumbua timu yoyote kwa sasa,”alisema Zahera.
Lakini ilibidi aweke wazi kuwa kashindwa kuipenya ngome ya akina wawa tu
ReplyDeleteNgome isiyopenyeka bongo. Nje ni uchochoro tu.
DeletePale mechi na SSC alikutana na muziki munene, so isingelikua kazi nyepesi kwake.
ReplyDeleteMziki mnene bongo. Ukitoka nje unakuwa mziki nyanya
Delete