February 21, 2019


KATIKA kuhakikisha wanaweka mambo sawa ndani ya Klabu ya Yanga, Wabunge wanne wameteuliwa kuungana na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake, Malangwe Mchungahela kuanza mchakato upya.

Wabunge ambao wameteuliwa kwa ajili ya kuunda kamati ya uchaguzi ya Yanga ni pamoja na Venance Mwamoto, Seifu Hamisi Gulamali, Dastan Kitandula na Saidi Mtanda.

Awali Yanga ilipanga kufanya uchaguzi wake mkuu Januari 13, mwaka huu, ulioandaliwa na TFF, uchaguzi ambao ulipingwa na baadhi ya wanachama kutoka katika mikoa minne tofauti kutokana na kuendelea kumtambua aliyekuwa mwenyekiti wake, Yusuf Manji.

Aidha uchaguzi huo ulikuwa ufanyike kwa lengo la kuziba nafasi ya viongozi waliojiuzulu akiwemo Manji na makamu wake Clement Sanga na wajumbe kadhaa ambapo hadi sasa klabu hiyo imebakiwa na viongozi wanne pekee.

Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo, alisema wabunge hao wanne wameteuliwa kwa ajili ya kuungana na kamati ya uchaguzi ya TFF kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati ya uchaguzi ili waandae uchaguzi upya.

“Tayari wabunge wanne wameteuliwa ambao ni Gulamali, Mwamoto, Kitandula na Mtanda ambao wataungana na kamati ya uchaguzi ya TFF ambapo watakutana kwa ajili ya kupanga mkakati wa uchaguzi upya ila haijajulikana utapangwa lini,” alisema Siza.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic