February 21, 2019


KOCHA wa Dodoma FC, inayopambania kucheza ligi kuu msimu ujao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema licha ya uwezo wa Mbukinafaso, Zana Coulibaly ambao ameonyesha hivi karibuni, lakini hawezi kumfunika Shomary Kapombe.

Kapombe yupo nje ya uwanja kwa miezi kadhaa sasa akiuguza majeraha ya mguu aliyopata wakati akitumikia Taifa Stars, ambapo klabu yake ya Simba ilichukua jukumu la kumsajili Zana aje kuwa mbadala wake kwa kipindi hiki ambacho yuko majeruhi.

Zana ameonesha uwezo wa hali ya juu kwenye mechi kubwa mbili alizocheza hivi karibuni, akiisaidia timu hiyo kupata ushindi kwenye michezo mitatu mfululizo dhidi ya Mwadui, Yanga na Al Ahly ya Misri.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Julio alisema kuwa, watu wasimfananishe Kapombe na Zana kwani watakuwa wanamnyima haki ya msingi mchezaji huyo.

“Nchi mzima inamjua Kapombe ni mchezaji wa aina gani, kwa hiyo mnapoamua kumfananisha na mchezaji mwingine muwe na pointi za kutosha.

“Yule Kapombe atakupa vitu vingi kwa wakati mmoja, atakaba, atafunga, atapiga krosi na atafanya kila kitu uwanjani.Huyo Zana mwambieni atafute namba nyingine akacheze siku Kapombe atakaporejea,” alisema Julio.

5 COMMENTS:

  1. Huyu Julio ndio kocha wa Simba kwa sasa?
    Atakayecheza atateuluwa ba kocha na sio Julio.
    Yeye akazabe na Dodoma United au imemshinda?
    Wakati mwingine ni bora kufunga mdomo.

    ReplyDelete
  2. Napingana na mtizamo wa Julio juu ya uwewzo Zana coulibali na kapombe. Kapombe kweli kabisa ni mchezaji wa aina yake.kwanza kabisa sifa moja ya kapombe ni kujitoa katika ufanyaji wa kazi yake yaani nu machezaji mwenye kujituma bila ya uoga ila Zana yupo zizuri zaidi kwenye nafasi hiyo hasa linapokuja suala la physical. Zana yupo fit zaidi ya Kapombe. Nasikia ni kiraka pia kama kapombe sijui yeye na kapombe nani mzuri zaidi kwenye nafasi nyengine. Kapombe ni kiungo asilia hasa kiungo wa nchini na atakaporudi ni faraja kubwa kwa diffence ya Simba.

    ReplyDelete
  3. Nina imani Wote wawili wanaweza kucheza kwa wakati mmoja na wakatengeneza Simba imara zaidi. Kocha anaweza kufanya hivyo. Wachezaji hawa wawili wote ni wazuri sana. Mfumo ndio utakaoibeba Simba katika kuwatumia wote wawili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic