February 21, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa wachezaji wake wote wa Yanga wanajuhudi uwanjani na anawependa ila anakubali uwezo wa chipukizi mmoja anayekuja kwa kasi.

Zahera amesema amekuwa na wachezaji muda mwingi hasa kwenye mazoezi pamoja na mechi ila anakubali zaidi uwezo wa Boxer ambaye ni beki kwenye kikosi cha kwanza.

"Wote wachezaji wazuri na ninawapenda ila ninavutiwa na uwezo wa Paul Godfery, huyu bado kijana na anajuhudi akiwa uwanjani.

"Naamini atakuja kufanya mambo makubwa zaidi hapo baadaye iwapo ataendela kufuata maelekezo na kujituma kila siku," amesema.

Boxer alikuwa anachezea Yanga B alipandishwa kikosi cha kwanza baada ya Juma Abdul ambaye ni nahodha msaidizi kupata majeraha licha ya kurejea kwenye kikosi bado Boxer ameendelea kuaminiwa na Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic