February 21, 2019



SIKU zote hizo alizocheza Azam, Obrey Chirwa hakufunga bao kwenye ligi lakini sikuchache kabla ya mechi ya Simba anaanza mambo yake.

Chirwa amejiunga na Azam msimu wa dirisha dogo akitokea Misri imemlazimu kusubiri zipite dakika 682 kufungua akaunti ya mabao.

Chirwa ambaye awali alikuwa anaitumikia Yanga na msimu wa 2017/18 alifunga mabao 12 kwenye ligi kabla ya kwenda Misri timu ya Nogoom FC kucheza alirejea tena Bongo baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo.

Akiwa Azam FC amecheza michezo saba bila ya kufunga zaidi ya kuishia kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo wao dhidi ya Alliance.

Kwenye mchezo wa nane Chirwa anafungua akaunti yake ya mabao kwa kufunga bao la kwanza msimu huu kwenye ligi baada ya kujiunga na Azam FC walipolazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic